NEWS

Monday, 21 April 2025

Kichapo cha 4G toka kwa Yanga, Kocha wa Fountain Gate atupa lawama kwa golikipa wake



Kocha wa Fountain Gate FC, Robert Matano (kushoto) na Kipa wa timu hiyo, John Noble.
--------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Babati

Baada ya kuchezea kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Yanga SC "wananchi", Kocha wa Fountain Gate FC, Robert Matano, ametupa lawama kwa mlinda lango wa timu hiyo, John Noble, kwamba makosa yake yaliitoa timu mchezoni na kusababisha kupoteza mchezo huo.

Matano ametupa lawama hizo kwa golikipa wake alipofanyiwa mahojiano na chombo cha habari muda mfupi baada ya kutamatika kwa mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC leo Jumatatu jioni kwenye Uwanja wa Tanzanite, Babati mkoani Manyara.

"Amekuwa akifanya vizuri lakini leo ametuangusha, kwa kipa mkubwa wa kariba yake kufanya makosa ya namna ile ametugharimu na kututoa kwenye mchezo kabisa," Matano amesema akionesha kusikitishwa sana na kitendo hicho.

Kutokana na kukasirishwa na kiwango kibovu cha Noble, kocha huyo alilazimika kumtoa mchezoni mwishoni mwa kipindi cha kwanza kumpisha Rashid Parapanda ambaye alidaka mpaka mwisho wa mchezo huo na kuruhusu pia magoli mawili.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages