NEWS

Monday, 21 April 2025

Papa Francis afariki dunia, Vatican yatangaza



Papa Francis enzi ya uhai

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, alifariki dunia leo Jumatatu ya Pasaka, Aprili 21, 2025, akiwa na umri wa miaka 88 katika makazi yake yaliyopo Casa Santa Marta, Vatican.

Muda mfupi uliopita, Mwadhama, Kardinali Farrell, ametangaza kwa masikitiko kifo cha Baba Mtakatifu Francis, kwa maneno haya:

"Ndugu wapendwa, kwa huzuni kubwa sina budi kutangaza kifo cha Baba Mtakatifu Francisko''.

Saa 7:35 asubuhi ya leo (saa za huko), Askofu wa Roma, Francis, alirudi nyumbani kwa Baba. Maisha yake yote yaliwekwa wakfu kwa huduma ya Bwana na Kanisa Lake."

"Alitufundisha kuishi maadili ya Injili kwa uaminifu, ujasiri na upendo wa ulimwengu wote, hasa kwa ajili ya maskini zaidi na waliotengwa zaidi."

Farrell ameongeza: "Kwa shukrani nyingi sana kwa ajili ya kielelezo chake kama mfuasi wa kweli wa Bwana Yesu, tunaipongeza roho ya Papa Francisko kwa upendo wa huruma usio na kikomo wa Mungu Mmoja na wa Utatu."

Kifo cha Papa kimekuja chini ya saa 24 baada ya kujitokeza kwenye Uwanja wa St Peter's Square mjini Vatican kwa ajili ya Jumapili ya Pasaka jana.

Alitoka akiwa kwenye kiti cha magurudumu na kupunga mkono kutoka kwenye baraza ya Basilica ya St Peter's kwa umati wa watu waliokuwa wakishangilia na kusema: "Ndugu wapendwa, Pasaka njema."

Chanzo: BBC Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages