NEWS

Sunday, 27 April 2025

Tarime: Nyambari Nyangwine aahidi kuchangia Kwaya ya SDA Itiryo shilingi milioni tano



Kwaya ya Goodness ya Kanisa la SDA Itiryo ikiimba moja ya nyimbo zao wakati wa harambee ya kuchangia ununuzi wa vifaa vyake iliyofanyika kanisani hapo jana Jumamosi, ambapo Nyambari Nyangwine aliahidi kuichangia shilingi milioni tano.
-------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Tarime

Mwandishi, mchapishaji na msambazaji wa vitabu maarufu nchini, Nyambari Nyangwine, ameahidi kuipiga jeki Kwaya ya Goodness ya Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) la Itiryo wilayani Tarime, Mara.

Nyambari ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime kwa tiketi ya chama tawala - CCM, ameahidi kuichangia kwaya hiyo shilingi milioni tano katika harambee ambayo aliwakilishwa na Fred Mariba kama mgeni rasmi.

Harambee hiyo ilifanyika kanisani hapo jana Jumamosi kwa lengo la kupata fedha za kununua vifaa muhimu vya kwaya hiyo.


Fred Mariba akizungumza katika harambee hiyo.

“Nyambari ni mtu mkarimu, anapenda kazi ya Mungu, amesema atawachangia shilingi milioni tano,” alisema Mariba ambaye naye aliahidi kumuunga mkono Nyambari kwa kuichangia kwaya hiyo shilingi laki tano.

Kwa upande wake, Mchungaji wa Kanisa la SDA Itiryo, Mussa Magau, alimshukuru Nyambari Nyangwine kwa kuitikia wito na kukubali kuchangia fedha za ununuzi wa mahitaji muhimu ya kwaya hiyo.

“Tunamuombea Nyambari Nyangwine, Mwenyezi Mungu azidi kumuongezea ili alipotoa aongezewe,” alisema Mchungaji Magau.

Huo ni mwendelezo wa utamaduni ambao Nyambari Nyangwine amejijengea wa kujitolea kuchangia maendeleo ya shughuli za kiroho kwenye madhehebu mbalimbali ya dini wilayani Tarime.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages