![]() |
Dkt Rhimo Simeon Nyansaho |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt Rhimo Simeon Nyansaho kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF).
Taarifa fupi iliyotolewa jana Jumatatu Mei 26, 2025, na Ikulu jijini Dodoma ilisema kuwa Dkt Nyansaho anachukuwa nafasi ya Dkt Abdul Razack Badru ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).
Kabla ya uteuzi wa jana, Dkt Nyansaho alikuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania.
Naye Dkt Badru amechukua nafasi ya Dkt Elirehema Joshua Doriye ambaye uteuzi wake wa Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA umetenguliwa na Rais.
No comments:
Post a Comment