NEWS

Tuesday, 3 June 2025

Serikali yalifuta Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Gwajima



Askofu Josephat Gwajima

Na Mwandishi Wetu

Serikali imelifuta rasmi Kanisa la Ufufuo na Uzima linalomilikiwa na Askofu Josephat Gwajima nchini kwa "kuhatarisha amani na utulivu nchini".

Taarifa iliyotolewa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia jana jijini Dodoma imeeleza kwamba hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu katika siku za karibuni Askofu Gwajima amekuwa akijihusisha na "mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya kuchonganisha serikali na wananchi".

Taarifa hiyo imeeleza kuwa vitendo hivyo vya Askofu Gwajima, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe, mkoani Dar es Salaam, ni kinyume cha Sheria ya Jumuiya.

"Hivyo kwa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu 17 (b) cha Sheria ya Jumuiya, nakujulisha kuwa nimefuta usajili wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (Glory of Christ Tanzania Church) kuanzia leo tarehe 02 Juni 2025. Unatakiwa kusitisha shughuli za kanisa lako mara moja," taarifa ilisema.

Taarifa ilieleza kuwa Jumuiya ya Kiraia iliyofutiwa usajili wake ina haki ya kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kupinga uamuzi wa kufutwa.

Rufaa ya kupinga kufutwa kwa kanisa hilo inatakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndaniya ya Nchi siku 21 kuanzia tarehe ya uamuzi wa kuondolewa kwenye orodha ya usajili wa Jimuiya za Kiraia.

Askofu Gwajima allingia kwenye ulingo wa siasa mwaka 2020 alipogombea Ubunge jimbo la uchaguzi la Kawe na kuibuka mshindi.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi linaelezwa kuwa limelizingira eneo la kanisa la Ufufuo na Uzima baada ya taarifa ya kufutwa kwake kwenye orodha ya Jumuiya za Kiraia zilizosajiliwa na serikali kupotia Wizara ya Mambo ya Ndani.

Tukio la kuzingirwa kwa kanisa hilo lilifanyika usiku wa kuamkia leo na waumini wachache waliokutwa kwenye kanisa hilo walipigwa butwaa walipowaona polisi - baadhi wakiwa wamevaa sare zao na wengine mavazi ya kiraia.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages