NEWS

Tuesday, 12 August 2025

DC Mkuchika ahamasisha vijana mkoani Mara kushiriki Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025



Mkuu wa Wilaya (DC) ya Butiama, Thecla George Mkuchika (katikati waliokaa), katika picha ya pamoja na viongozi na vijana walioshiriki Kongamano la Vijana Mkoa wa Mara wilayani Butiama leo.
------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Butiama

Mkuu wa Wilaya (DC) ya Butiama mkoani Mara, Thecla George Mkuchika, amewahamasisha vijana wa mkoa huo kushiriki kikamilifu katika Mbio za Kitaifa za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika mkoani Mara kuanzia Agosti 15 hadi 23, 2025.

Mkuchika ameyasema hayo katika hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Vijana wa mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa yaliyofanyika kimkoa wilayani Butiama leo Agosti 12, 2025.


Aidha, DC huyo ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi,  katika kongamono hilo, amewahamasisha vijana kushiriki Uchaguzi Mkuu ujao ili kuchagua viongozi bora watakaosimamia rasilimali za taifa na kuleta maendeleo.

Pia, amewahamasisha vijana kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika mkoa wa Mara, zikiwemo za kilimo, uchimbaji wa madini, uvuvi na ufugaji.

Kongamano hilo la Vijana wa Mkoa wa Mara limefadhiliwa na Shirika la Powerlife, likiwa na kaulimbiu inayosema: "Nguvu ya Vijana Tanzania kwa Maendeleo Endelevu."
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages