NEWS

Sunday, 31 August 2025

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM aahidi neema Tarime Vijijini akihutubia mkutano wa kampeni Nyamongo



Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi (aliyevaa miwani) akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, Marwa Daudi Ngicho, alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni mjini Nyamongo leo AGOSTI 31, 2025. Wengine ni MNEC Christopher Mwita Gachuma (wa pili kulia mbele) na Mkuu wa Wilaya, Meja Edward Gowele (wa kwanza kulia mbele).
-------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Nyamongo

Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, leo Agosti 31, 2025 ameendelea na kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa kuhutubia mkutano mkubwa wa wananchi katika mji wa Nyamongo, jimbo la Tarime Vijijini, mkoani Mara.

Balozi Dkt. Nchimbi amewaomba wananchi kumchangua Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Oktoba 29, 2025.

Pia, amewanadi wagombea wa chama hicho wa nafasi za ubunge na udiwani katika majimbo na kata za mkoa wa Mara, akiwemo Mwita Waitara anayegombea ubunge wa jimbo la Tarime Vijijini na Godfrey Kegoye anayegombea udiwani wa kata ya Matongo iliyopo Nyamongo.

“Dkt. Samia na mimi [Dkt. Nchimbi], wabunge na madiwani tuko tayari kuwatumikia, tarehe 29 [Oktoba 2025] tuchagueni kwa kura nyingi,” amesema mgombea mwenza huyo wa urais.


Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi (kushoto) akiwanadi Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara (katikati) na Mgombea Udiwani Kata ya Matongo, Godfrey Kegoye, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Nyamongo.
-----------------------------------------


Wananchi wakimshangilia Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani), wakati akihutubia mkutano wa kampeni za Chaguzi Mkuu katika mji wa Nyamongo leo.
---------------------------------------

Pamoja na maendeleo mengine, Balozi Dkt. Nchimbi amesema Serikali ya CCM itaendeleza ujenzi wa barabara za lami na uboreshaji wa huduma za afya, elimu na maji.

Ametaja barabara ambazo tayari zimeingizwa kwenye mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami ndani ya miaka mitano ijayo kuwa ni pamoja na Tarime-Mogabiri (km 9.3), Mogabiri-Nyamongo (km 25), Namongo-Mugumu (km 45) na Tarime-Mugumu (km 89).

Balozi Dkt. Nchimbi ambaye ameambatana na wenyeji wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi na Mwenyekiti wa chama hicho, Marwa Daudi Ngicho, pia alihutubia mikutano mikubwa ya kampeni katika majimbo ya Tarime Mjini na Rorya.


Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa, wakiteta na kufurahia jambo katika mkutano wa kampeni Nyamongo.
---------------------------------------


Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akimwombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini kupitia CCM, Esther Matiko, kwenye mkutano wa kampeni jimboji humo leo.
----------------------------------------------
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages