
Kimberly Cheatle
------------------------
Mkurugenzi wa idara ya ulinzi wa viongozi (Secret Service), Kimberly Cheatle, amejiuzulu, siku moja baada ya kukiri kuwa idara hiyo ilishindwa katika dhamira yake ya kuzuia jaribio la mauaji dhidi ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Cheatle alikuwa akikabiliwa na shinikizo kutoka kwa viongozi wa vyama viwili vikubwa nchini humo ajiuzulu baada ya mtu mwenye bunduki, mwenye umri wa miaka 20 kumjeruhi Trump mgombea wa sasa wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican katika mkutano wa kampeni wa Julai 13 mjini Butler, Pennsylvania.
Cheatle alifika mbele ya kamati ya bunge siku ya Jumatatu na kusema kuwa shambulizi dhidi ya Trump, ambaye alijeruhiwa kidogo kwenye sikio lake la kulia, lilikuwa kushindwa kwa idara hiyo ya Secret Service.
Warepublican na Wademokrat walimtaka Cheatle ajiuzulu. Aliwakasirisha wabunge kutoka pande zote mbili kwa kukataa kutoa maelezo mahsusi kuhusu shambulio hilo, akitoa sababu ya kuwepo kwa uchunguzi unaoendelea.
Mshambuliaji huyo alimfyatulia risasi Trump kwa bunduki aina ya AR dakika chache baada ya kuanza kuwahutubia waliohudhuria hafla hiyo ya kampeni.
Akiwa juu ya paa la jengo lililo karibu, aliuawa kwa kupigwa risasi na afisa wa Secret Service chini ya sekunde 30 baada ya kufyatua risasi ya kwanza, kati ya nane zilizotumika.
Wabunge walimhoji Bi Cheatle kuhusu maandalizi ya usalama kabla ya mkutano wa kampeni wakati wa kikao cha saa sita cha Kamati ya Uangalizi ya Bunge.
Bi Cheatle alichukua jukumu la kudorora kwa usalama, lakini alionekana kukataa kabisauwezekano wake kujiuzulu.
Mashahidi waliripoti kumwona mshukiwa Thomas Matthew Crooks - akiwa na bunduki juu ya paa kwenye mkutano huo dakika chache kabla ya risasi kufyatuliwa.
Maafisa wa usalama na watekelezaji sheria kutoka kwa vyombo mbalimbali walikuwepo kwenye mkutano huo.
Wakati wa ushuhuda wake, Bi Cheatle hakuwapa wabunge habari yoyote mpya kuhusu jinsi Crooks alivyoweza kufikia paa ambapo alikuwa amelala na kwa nini Trump aliruhusiwa kupanda jukwaani.
Chanzo: BBC
UNAWEZA PIA KUSOMA:
- 1. Mwenge wa Uhuru kuwasili Mara kesho, kukagua miradi ya bilioni 25/-
- 2.TIC watembelea kahawa ya Tarime inayotamba soko la dunia
- 3.Oparanya na wenzake ‘wala shavu’ Baraza jipya la Mawaziri la Rais Ruto
- 4.Nyambari akutana na Spika wa Bunge la Tanzania jijini New Delhi
- 5.Mwenyekiti UWT CCM Mara ahamasisha wanawake wilayani Tarime kugombea uongozi, wavuna wanachama wapya
- 6.Balozi Mbarouk amwandikia Spika barua ya kujiuzulu ubunge
- 7.Maswi, Ridhiwan wang’ara teuzi za Rais Samia, Nape na Makamba wavuliwa uwaziri, Mashinji na Afraha wahamishwa Serengeti
No comments:
Post a Comment