NEWS

Wednesday, 24 July 2024

Oparanya na wenzake ‘wala shavu’ Baraza jipya la Mawaziri la Rais Ruto



Rais William Ruto
--------------------------

Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto amewateua baadhi ya viongozi wa upinzani kuingia katika Baraza lake jipya la Mawaziri.

Ruto pia amewarejesha mawaziri wa zamani wanne waliokuwa katika Baraza lake la awali, akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Sheria, Justin Muturi.

Mawaziri walioteuliwa kutoka vyama vya upinzani kikiwemo ODM na wizara zao zikiwa kwenye mabano, ni pamoja na Hassan Joho (Madini), John Mbadi (Fedha), Stella Langat (Jinsia) na Wycliffe Oparanya (Vyama vya Ushirika).

Mbali na hao wa upinzani, wengine walioteuliwa kuwa mawaziri katika Baraza jipya la Rais Ruto, ni Salim Mvurya (Uwekezaji), Rebecca Miano (Utalii), (Opiyo Wandayi (Nishati), Kipchumba Murkomem (Vijana na Michezo), Alfred Mutua (Kazi) na Justin Muturi (Utumishi wa Umma).
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages