Rais Ruto |
Rais William Ruto ametangaza mawaziri kumi na moja kati ya 22 katika baraza lake la mawaziri.
Katika hotuba yake kwa taifa , rais Ruto amesema kwamba idadi ya mawaziri waliosalia itatangazwa wiki ijayo baada ya mashauriano.
Haya yanajiri baada ya shinikizo kuongezeka kwa Rais kuchagua watu wenye uwezo ambao watamsaidia kutekeleza ajenda yake.
Rais amesema kwamba uteuzi huo ambao ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali - unafuatia mashauriano katika sekta ya kisiasa katika jaribio la kurudisha amani na utulivu nchini.
Orodha hiyo pia ilikuwa na Mawaziri sita waliofukuzwa kazi, ambao sasa wanarejea katika wizara tofauti, huku Prof. Kithure Kindiki, Alice Wahome na Adan Duale wakiendelea kushikilia nafasi zao za zamani.
Mawaziri walioteuliwa ni:
1.Kithure Kindiki - Waziri wa masuala ya Ndani
2.Dkt. Debra Mulongo Barasa - Waziri wa Afya
3.Alice Wahome - Waziri wa Ardhi
4.Aden Duale - Waziri wa Ulinzi
5.Davis Chirchir - Waziri wa Uchukuzi
6.Rebecca Miano - Mwanasheria Mkuu
7.Soipan Tuya - Waziri wa Mazingira
8.Julius Migosi - Waziri wa Elimu
9.Eric Muriithi - Waziri wa Maji
10.Dr Margaret Ndungu- Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia
11.Andrew Karanja - Waziri wa Kilimo
Wateule wapya watalazimika kuchunguzwa kabla ya kuzingatiwa ili kuidhinishwa na bunge kama Mawaziri.
"Ninaendelea kufanya mashauriano katika sekta mbalimbali kuhusu usawa wa Baraza la Mawaziri ambalo nitaliteua hivi karibuni. Mashauriano yapo katika hatua ya juu na michakato ya ndani katika sekta mbalimbali inaendelea ili kuwezesha uteuzi wangu wa uwiano wa Baraza hili la Mawaziri,” alisema Rais.
Uteuzi huo unajiri huku kukiwa na mgawanyiko mkubwa katika Muungano wa upinzani nchini Azimio ambapo baadhi ya viongozi wamepinga kuhusu kufanyika kwa mazngumzo yoyote yatakayopelekea baadhi ya viongozi wao kuorodheshwa katika baraza hilo.
CHANZO:BBC
UNAWEZA PIA KUSOMA:
- 1.Nyambari Nyangwine awasili India, atangaza bidhaa za Tanzania
- 2.Sababu za Halmashauri ya Serengeti kupata hati ya ukaguzi yenye mashaka
- 3. Musoma Vijijini wanavyopiga hatua ujenzi shule za sekondari za kata
- 4.Mwanahabari kumlipa fidia Waziri Mkuu wa Italia baada ya kufanya mzaha juu ya kimo chake
- 5.Rais Samia atembelea Sekondari ya Seminari ya Kaengesa mkoani Rukwa
- 6. HAIPPA PLC inavyoshagihisha uwekezaji Tanzania
No comments:
Post a Comment