NEWS

Friday 26 July 2024

Mwenge wa Uhuru wamkutanisha Sabaya na wananchi wa Serengeti aliowahi kuwaongoza kama DC



Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya (kulia) akionekana mwenye furaha alipokutana na Mwenyekiti mwenzake wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa wakati wa mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru, yaliyofanyika Robanda wilayani Serengeti mapema leo asubuhi. Sabaya aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti kwa miaka kadhaa. (Picha na Mara Online News)
----------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Serengeti
------------------------------------------

Milima haikutani. Ndivyo tunavyoweza kuelezea tukio la Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya kukutana na wananchi wa wilaya ya Serengeti aliyowahi kuiongoza kama Mkuu wa Wilaya (DC) kwa miaka kadhaa katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Sabaya ameambatana na viongozi wengine kutoka mkoa wa Arusha kukabidhi Mwenge wa Uhuru mkoani Mara, katika tukio lililofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Robanda wilayani Serengeti, mapema leo Julai 26, 2024 asubuhi.

Sabaya anakumbukwa kwa kuiongoza wilaya ya Serengeti kwa mafanikio makubwa, yakiwemo ya ujenzi wa shule za sekondari, kupambana na ujangili na kutokomeza wizi wa mifugo.

Viongozi walioshiriki katika mapokezi hayo ya Mwenge wa Uhuru ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Gerald Musabila Kusaya, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa, Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti, Angelina Marko na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara, Mary Daniel Joseph, miongoni mwa wengine.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya (wa pili kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi walipokutana katika mapokezi ya Mwenye wa Uhuru wilayani Serengeti leo. Anayefurahi katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa, na kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara, Mary Daniel Joseph. (Picha na Mara Online News)
-------------------------------------------------
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages