NEWS

Monday, 21 October 2024

Korea kusini yamuweka kiti moto balozi wa Urusi



 
Korea Kusini imemwita balozi wa Urusi, ikitaka "kuondoka mara moja" kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini ambayo inasema wanapewa mafunzo ya kupigana nchini Ukraine.

Takriban wanajeshi 1,500 wa Korea Kaskazini, wakiwemo wale wa kikosi maalum tayari wamewasili nchini Urusi, kwa mujibu wa shirika la kijasusi la Seoul. 

Katika mkutano na balozi Georgiy Zinoviev, makamu wa waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini Kim Hong-kyun alishutumu hatua hiyo na kuonya kwamba Seoul "itajibu kwa hatua zote zinazowezekana". 
 
Bw Zinoviev alisema atawasilisha jambo hilo, lakini akasisitiza kuwa ushirikiano kati ya Moscow na Pyongyang "uko ndani ya mfumo wa sheria za kimataifa". 

Haijulikani alikuwa akimaanisha ushirikiano gani. Balozi huyo hakuthibitisha madai kuwa Korea Kaskazini imetuma wanajeshi kupigana na jeshi la Urusi. 

Pyongyang pia haijazungumzia madai hayo.Korea Kusini kwa muda mrefu imekuwa ikiishutumu Kaskazini kwa kusambaza silaha kwa Urusi kwa ajili ya matumizi katika vita dhidi ya Ukraine, lakini inasema hali ya sasa imevuka uhamishaji wa vifaa vya kijeshi.

Baadhi ya ripoti za vyombo vya habari vya Korea Kusini vimesema kuwa wanajeshi 12,000 wa Korea Kaskazini wanatarajiwa kutumwa. "Hii sio tu inatishia sana Korea Kusini lakini jumuiya ya kimataifa," Kim alisema Jumatatu. 

Moscow na Pyongyang zimeongeza ushirikiano baada ya viongozi wao Vladimir Putin na Kim Jong Un kutia saini mkataba wa usalama mwezi Juni, wakiahidi kuwa nchi zao zitasaidiana iwapo kutatokea "uchokozi" dhidi ya nchi yoyote ile.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages