NEWS

Monday, 18 November 2024

Kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo: Rais Samia aagiza majengo yote yakaguliwe



Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akizungumza kutoka Rio de Janeiro, Brazil.

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amemwagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuongoza timu ya ukaguzi wa majengo yote Kariakoo, Dar es Salaam na kutoa taarifa ya jinsi yalivyo, baada ya shughuli za uokozi kwenye ghorofa lililoporomoka katika eneo hilo juzi.

Rais pia amelitaka Jeshi la Polisi kupata taarifa kamili kutoka kwa mmliki wa jengo lililoporomoka ili kujua ujenzi wake ulivyofanyika.

Alitoa maagizo hayo jana Novemba 17, 2024 akiwa Rio de Janeiro, Brazil anakohudhuria mkutano wa mataifa tajiri duniani - G20.

Rais Samia alitumia nafasi hiyo pia kutuma salaam za pole kwa wafiwa, ndugu na jamaa za watu waliokufana kujeruhiwa kwenye tukio la kuporomoka kwa jengo hilo.

Alisema serkali itabeba jukumu la tiba kwa majeruhi na waliopoteza maisha yao watazikwa kwa heshima inayostahili.

Aidha, Rais Samia aliwapongeza wananchi wote, vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi binafsi zilizoshiriki kwenye shughuli za uokozi.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages