NEWS

Tuesday, 19 November 2024

Mara: Dkt Biteko kuzindua kampeni za CCM Nyamongo



Dkt Doto Biteko

Na Mwandishi Maalumu/ Mara Online News

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko kesho Novemba 20, 2024 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara kwa ajili Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Mgeni rasmi katika uzinduzi wa huo atakuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Doto Biteko,” Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Noverty Kibaji ameiambia Mara Online News ofisini kwake mapema leo asubuhi.

Dkt Biteko pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

Kwa mujibu wa Kibaji, uzinduzi huo utafanyika kimkoa wilayani Tarime katika kata ya Matongo iliyopo mji mdogo wa Nyamongo, jirani na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.

Ametoa wito kwa wananchi, wanachama wa CCM, wapenzi, wakereketwa wa chama hicho tawala kujitokeza kwa wingi kuhudhuria uzinduzi huo ambao unatarajiwa kubadilisha siasa za Nyamongo kuwa za kijani, kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya siasa wilayani Tarime.

Kibaji amesema maandalizi yote ya uzinduzi huo ambao utaanza saba mchana yanakawenda vizuri.

Uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mtaa umepangwa kufanyika Novemba 27, 2024 kote nchini.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages