
Raila Odinga
Na Mwandishi Wetu
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga amekubali kushindwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti, Mahmoud Ali Youssouf katika kinyang’anyiro cha uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).
Akizungumza na vyombo vya habari juzi baada ya uchaguzi huo jijini Addis Ababa, Ethiopia, Raila alimpongeza Youssouf kwa kuibuka mshindi.
“Ninakubali matokeo ya kura. Kwa hivyo, mimi mwenyewe ninakubali kushindwa. Wanasema kwamba lazima tuimarishe demokrasia katika bara la Afrika na ninataka tutumie hii kama mfano mwema.
"Hivyo basi, namtakia mshindani wangu Mahmoud Ali Youssouf kila la kheri. Namtakia mafanikio katika kazi yake,” Raila alisema.
Aidha, aliwashukuru waliompigia kura na ambao hawakumpigia akisema wametumia vyema haki zao za kidemokrasia.
“Sina machungu. Nina furaha sana, na kama haitoshi, bado ninapatikana kutoa huduma yoyote kwa bara hili katika uwezo mwingine wowote,” alisema.

Mahamoud Ali Youssouf
Mgombea Mahamoud Ali Youssouf kutoka Djibouti alishinda kwa kura 33 katika raundi ya saba ya upigaji kura baada ya Raila kujiondoa katika raundi ya sita aliposhindwa na Youssof katika raundi ya tano na ya sita.
Kwa upande wake mgombea kutoka Madagascar, Richard Randriamandrato aliondoka kinyang'anyironi mapema baada ya kushika mkia kwenye raundi wa kwanza, pili na tatu.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Raila Odinga alivyoukosakosa uenyekiti Tume ya Umoja wa Afrika
>>Taasisi ya Nyambari Nyangwine yazifikia kata za Manga, Kibasuka na Kiore kwa msaada wa vitabu vya sekondari
>>Tarime: Heche kuchinja ng’ombe 20 kujipongeza kwa ushindi CHADEMA
>>Mwanafunzi wa sekondari afa kwa kugongwa na basi la Kisire Tarime
No comments:
Post a Comment