![]() |
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan |
Na Mwandishi Wetu
Rais Samia Suluhu Hassan amewapangia vituo vya kazi mabalozi wawili ambao wataiwakilisha Tanzania katika nchi za Msumbiji na Sweden.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Ikulu kutoka Pemba, Balozi Hamad Khamis Hamad ataiwakilisha Tanzania katika nchi jirani ya Msumbiji ambayo wapigania uhuru waje waliishi Tanzania wakati wa harakati za ukombozi wa kuwang"oa watawala wa Kireno walioitwala nchi hiyo kwa karne tano.
Balozi Mobhare Holmes Matinyi ataiwakilisha Tanzania huku Sweden, nchi ambayo imetoa misaada mingi ya maendeleo tangu miaka ya mwanzo ya Tanganyika huru iliyokuwa chini ya himaya ya Waingereza.
Katika hatua nyingine, kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, Rais Samia amemteua Rachel Stephen Kasanda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi kuchukua nafasi ya Lauteri John Kanoni ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Rais pia amemteua Jafari Ramadhani Kideghesho kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania.
Naye CPA Ashraph Yusuph Abdulkarim ameteuliwa kuwa Meneja Mkuu wa Masoko Kariakoo.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
»Rais Samia atoa milioni 100/- kusaidia waathirika wa maafa ya mvua Musoma Mjini
»Mfanyabiashara na Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM aripotiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha
»Afisa Tarafa (Mstaafu) Machango “Aiko” afariki duniaMPYA
»Nyambari Nyangwine kufadhili semina ya washairi wa Tanzania ili kuboresha ufanisi wao
No comments:
Post a Comment